NEWS

2 Aprili 2019

VIDEO: MAKONDA KUKUTANA NA WAJANE APRILI 4, 2019 DAR

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amesema atakutana na kina mama wajane, jijini Dar es Salaam, Aprili, 4,  mwaka huu, ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili,  likiwemo suala la mirathi  na kutoa elimu kwao kuhusu fedha ambazo ni asilimia nne zinazotengwa kila manispaa kwa wanawake ili wajue kuwa fedha hizo zinawahusu.

 

Makonda ameyasema hayo ofisini kwake leo akiongea na waandishi wa habari.

 

Pia amepongeza wakuu wa wilaya za Ilala na Temeke kwa kukamilisha zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo-wadogo kwenye maeneo yao,  na amewataka wakuu wa wilaya za Kigamboni, Kinondoni na Ubungo kuongeza kasi ya kukamilisha zoezi hilo.

The post VIDEO: MAKONDA KUKUTANA NA WAJANE APRILI 4, 2019 DAR appeared first on Global Publishers.