NEWS

30 Aprili 2019

Waziri aeleza kuongeza Maaskari Uchaguzi Mkuu

Serikali imesema iko tayari kuongeza idadi ya Askari polisi wa kulinda usalama kwenye Uchaguzi Mkuu Visiwani Zanzibar kwa kile ilichokieleza kuwa ikifikia kipindi cha Uchaguzi kumekuwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa sheria unaosababaishwa na Chama Cha Kikuu cha Upinzani Visiwani humo CUF


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni, wakati akijibu swali la Mbunge Machano Othman Said Bungeni jijini Dodoma ambaye alihoji juu ya umuhimu wa kuongeza askari polisi kwenye kipindi cha Uchaguzi Mkuu na kupendekeza chaguzi hizo kutofautishwa ili kuepusha madhara.

Mbunge Machano alihoji kuwa, "Serikali ipo tayari kuongeza idadi ya askari wakati wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar? pia iko tayari kutenganisha Uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Tanzania bara?".

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hammad Masauni amesema suala la matukio ya kiuhalifu visiwani Zanzibar limekuwa likisababishwa na baadhi ya vyama vya upinzani visiwani humo akikitaja chama kikuu cha upinzani visiwani humo CUF.

"Serikali kweli iko tayari kuongeza idadi ya askari kwenye chaguzi, kwa sababu vyombo hivi vinafanya kazi kwa ushirikiano, kuhusiana na mabadiliko ya uchaguzi, suala hilo linazungumzika na hoja ya Mbunge ina mashiko", amesema Masauni.