NEWS

21 Mei 2019

RIDHIWANI AWABEBA WAZEE NA WENYE ULEMAVU, CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akimkabidhi msaada wa Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair), Mkazi wa Zomozi – Ubena, Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambaye ni mlemavu wa miguu, jana baada ya Mbunge huyo kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM wa Kata ya Ubena-Zomozi, Chalinze.

Ridhiwani akimuelekeza Mkazi wa Zomozi – Ubena, Mzee Cosmas Alphonce Chongwe, ambaye ni mlemavau wa Miguu namna ya kutumia Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair), aliyomkabidhi msaada huo.

Ridhiwani akimkabidhi fimbo maalum kwa ajili ya walemavu wa macho, Josephat Mgonge, ambaye ni mlemavu wa macho.

 Ridhiwani akikabidhi mfuko wa saruji kwa uongozi wa CCM, msaada wa mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza.

Ridhiwani akikabidhi kadi ya matibabu maalum kwa Wazee, Mzee Ally Gola, ambapo kadi 25 zilitolewa kwa wazee.

Mmoja wa wazee akimshukuru Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuwapatia msaada wa kadi za matibabu, kulia ni Diwani wa Kata ya Ubena – Zomozi, Nicholaus Muyuwa akishuhudia.

Baadhi ya wananchi.

The post RIDHIWANI AWABEBA WAZEE NA WENYE ULEMAVU, CHALINZE appeared first on Global Publishers.