NEWS

2 Agosti 2019

Aufungia mwili wa mtoto kwenye Friji kwa miaka 37


Mwanamke mmoja aleyejulikana kwa jina la Barbara mwenye umri wa miaka 68, anadaiwa kuweka mwili wa mtoto wake kwenye Friji kwa muda wa miaka 37.


Taarifa hizo zimetolewa na Mtoto wa Mama huyo aitwaye Adam Smith ambaye aligundua kuwa kuna Mwili kwenye Friji baada ya mama yake huyo kufariki Julai 21 mwaka huu.

Adam Smith amesema alihamia kwa Mama kabla hajafariki ili aweze kumsaidia kwa sababu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na ameeleza kuwa.

“Mama yake alikuwa ana sanduku ambalo alikuwa ameliweka kwenye Friji kwa muda wa mrefu sana, na yeye hakuwahi kulifungua hata siku moja, ila baada ya kulifungua aligundua kuna mtoto aliyegandishwa kwenye Friji, huku akiwa amefungiwa ndani ya ngozi yenye manyoya”

Aidha Adam Smith aliendelea kusema licha ya mwili  huo kukaa kwa muda mrefu kwenye Friji lakini bado ulikua una nywele, ngozi na pia ulikuwa unanyunyuziwa manukato.

Baada ya tukio hilo Adam Smith amesema Mama yake aliwahi kumwambia kuwa kuna ndugu yake ambaye alifariki kabla ya kuzaliwa yeye, Pia yupo tayari kutoa Vinasaba kwa Daktari na Polisi kwa uchunguzi zaidi.