Chama cha Wananchi CUF kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini hususani katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Sheria na haki za binadamu wa chama hicho, Salvatory Magafu ambapo amesema, ''tunamuomba Rais Magufuli kwa heshima na taadhima aruhusu, atoe tamko la kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa''.
Aidha Mkurugenzi huyo amelitaka jeshi la polisi nchini kuacha kukiuka sheria na lifanye kazi bila ubaguzi wala upendeleo ili kuendelea kulinda amani ya nchi.
Hatua hii imekuja baada ya chama hicho kuliandikia barua jeshi la polisi ya kuomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara Vingunguti relini, lakini baadae walipokea barua kutoka Ofisi ya Mkuu wa Polisi Buguruni ya kuzuia mkutano huo.