NEWS

5 Agosti 2019

Man City yaanza kazi, yabeba kombe la kwanza

MANCHESTER City wameanza kutwaa ubingwa wa kwanza msimu huu baada ya kuwachapa Liverpool kwa penalti 5-4 na kutwaa Ngao ya Jamii. Timu hizo zimefika kwenye mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1, kwenye Dimba la Wembley.

Liverpool walikuwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa Ngao hii kutokana na kufanya vibaya kwenye michezo ya maandalizi ya msimu.

Hata hivyo, walianza kwa kuwa nyuma baada ya Raheem Sterling kuanza kwa kuifungia City bao safi katika dakika ya 11 tu ya mchezo, lakini Sterling alikosa mabao mawili ya wazi akiwa na kipa baada ya kugongesha mwamba mara mbili. Sterling alifunga bao hilo baada ya uzembe wa mabeki wa Liverpool ambao walikuwa wanataka kuokoa mpira huo.

 

Kipindi cha pili, Liverpool walionekana kuamka na kuanza kulishambulia lango la City ambapo walijipatia bao la kusawazisha kupitia kwa Joel Matip katika dakika ya 77, ambaye alipata pasi kupitia kwa Van Djik.

Hata hivyo, Liverpool walikosa nafasi kadhaa za wazi kipindi cha pili cha mchezo huo na walikuwa wanaweza kupata mabao mengi kama wangezitumia vyema nafasi walizopata.

Hii ni mara ya sita City wanatwaa Ngao hiyo, ikiwa ni ya pili mfululizo, huku Liverpool wakibaki na mara zao 15. Liverpool walifunga penalti zao kupitia kwa Shaqiri, Adam Lalana na Oxlande Chamberlain, Mohammed Salah, huku Wijnaldum akikosa. Wakati City walifunga kupitia kwa Gundogan, Benando Silva, Oleksandar Zinchenko, Phil Foden na Jesus.

 

The post Man City yaanza kazi, yabeba kombe la kwanza appeared first on Global Publishers.