NEWS

4 Agosti 2019

Serikali Yazindua rasmi mpango wa Bima ya mazao mbalimbali


Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imezindua rasmi mpango wa Bima ya mazao mbalimbali ambao utaanza na wakulima wa zao la pamba Mkoa wa Simiyu na kahawa katika Mkoa wa Kagera.

Mpango huo umezunduliwa leo na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yanakoendelea maonyesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane).

Akizungumzia bima hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dk. Elirehema Doriye, amesema wakiwa kama watekelezaji wa mpango huo watahakikisha wakulima wote nchini wanapatiwa bima ya mazao yao.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameitaka NIC kuhakikisha wakulima wote wa mazao makuu matano wanajiunga na bima hiyo ili kuweza kubadilisha kilimo kuwa cha kisasa zaidi na chenye tija.