NEWS

30 Septemba 2019

Mpishi akamatwa kwa tuhuma za kutumia bangi kama kiungo cha kuongeza ladha


Mpishi mmoja amekamatwa kwa tuhuma za ulanguzi wa madawa ya kulevya baada ya polisi kugundua bangi nyumbani kwake. chefCARABINIERI CATANIA

Vyombo vya habari nchini Italia vimeripoti kuwa, Carmelo Chiaramonte ambaye ni mpishi anayeshiriki kipindi kwenye televisheni alipatikana na mimea miwili mikubwa ya bangi na kilo moja ya Indian hemp, polisi inasema.

Mvinyo uliochanganywa na bangi, zaituni, kahawa, na samaki aina ya tuna pia vilikusanywa nyumbani kwake karibu na Catania huko Sicily My ashariki.

Kwa mujibu wa BBC, Inaarifiwa mpishi huyo aliwaeleza maafisa wapolisi kwamba alikuwa anajaribu ‘viungo vipya vya upishi’.

Chiaramonte amesema yeye ni mshauri wa vyakula asili kwa upishi wa kileo “,

Mpishi huyo wa miaka 50, anayeishi katika kijiji cha Trecastagni, chini ya Mlima Etna ameachiwa huru huku kesi ikisubiriwa kuwasilishwa mahakamani.

Chiaramonte ni mpishi katika hoteli ya Katane Palace huko Catania.

Hupika vyakula vya watu wa Meditarenia kwa mujibu wa maelezo kwenye mtandao wake.

Alishiriki kipindi cha mapishi kwenye televisheni kuhusu “historia ya mazao na utamaduni wa kilimo cha Sicily”, La Sicilia limeripoti.

Mojawapo ya vipindi vyake kiliitwa ‘upishi uliokosa nidhamu’ na ‘vyakula vya kutia hamu ya tendo la ndoa’, gazeti hilo limesema.