NEWS

3 Oktoba 2019

Wambura Akiri Kosa, Aomba Msamaha

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura.

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabili.

 

Wambura amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa ameandika barua hiyo kufuatia ushauri uliotolewa na Rais John Pombe Magufuli kwa DPP.

 

Ameuomba upande wa mashtaka ufuatilie barua hiyo ili upate majibu kwa haraka. Baada ya maelezo hayo Wakili mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza mahakama kuwa watafuatilia suala hilo ili wapate majibu mapema na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 16, 2019.

 

Mshtakiwa anadaiwa kujipatia shilingi milioni 75 kutoka TFF wakati akijua kuwa fedha hizo siyo halali na zimetokana na shtaka la kughushi.

The post Wambura Akiri Kosa, Aomba Msamaha appeared first on Global Publishers.