NEWS

3 Oktoba 2019

Makaburi ya Marehemu wa Mlipuiko wa Mafuta Moro, Yaanza Kujengwa

HATIMAYE ujenzi wa ukuta unaozunguka makaburi ya ndugu zetu waliofariki kwenye ajari ya mlipuko wa Lori la Mafuta umeanza kujengwa.

 

Hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikaririwa na vyombo vya habari akipinga gharama ya shilingi milioni 30 ya kujenga ukuta huo iliyopengekezwa na wahusika waliopewa jukumu la kusimamika kazi hiyo.

”Eneo lile la makabuni ni nusu heka hivyo kiasi hicho cha millioni 30 ni kikubwa mno sisi kama serikali tutatoa million 10 kwa ujenzi wa ukuta huo” alikaririwa akisema Mh Waziri Mkuu wiki iliyopita alipofanya ziara mkoani hapa.

 

Kufuatia hali hiyo leo Mwandishi wa Mtandao huu aliamua kutinga kwenye makabuli hayo yaliyopo Kolla kwa lengo la kuchunguza kama ujenzi huo umeanza au la.

Mwandishi wa Mtandao huu ingawa leo hakuwakuta mafundi lakini alishuhudia kazi ya ujenzi wa ukuta huo ukianza kwa hatua za kuchimba msingi wa kiwango kizuri kuzunguka eneo lote la makaburi hayo sambamba na kushuhudia matilio ya Mchanga, Kokote na matofali yakiwa saiti.

 

Kwa kuwa hakuwepo mtu yoyote eneo hilo mtandao huu umeshindwa kubaini wasimamizi wa ujenzi huo pamoja na kampuni iliyopewa tenda ya kujenga ukuta huo, juhudi za Mwandishi wa habari hizi kuwatafuta wahusika hao ili wazungumzie ujenzi huo zinaendelea.

TUJIKUMBUSHE
Agosti 10 mwaka huu Lori lililobeba mafuta aina ya Petrol likitokea Dr kuelekea lringa lilipinduka Msamvu eneo la ltigi na kundi la wananachi walijitokeza kwa wingi kugema mafuta huku wengine wakidaiwa kuchomoa betri hali iliyodaiwa kusababaisha mlipuka mkali wa moto uliouwa watu 104.

Kundi kubwa la Marehemu hao walizikwa eneo hilo la makaburi ya Kolla huku baadhi waliotambuliwa na ndugu zao wakiende kuzikwa kwenye mikoa yao.

Waziri Mkuu aliyemwalikisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mazishi hayo aliagiza ujengwe ukuta kuzunguka makaburi hayo.

Na Dunstan Shekidele | GPL, Morogoro.

The post Makaburi ya Marehemu wa Mlipuiko wa Mafuta Moro, Yaanza Kujengwa appeared first on Global Publishers.