NEWS

19 Novemba 2019

Bongozozo Asikitishwa na Watu Wanaomtukana Mkewe Inbox


Mhamasishaji wa timu ya taifa Nicky Bongozozo, amemuomba msamaha Mke wake Caro Jessica, kwa kosa lake la kuongea kwa kupitiliza, hali iliyopelekea mkewe huyo kufuatwa na kutukanwa na watu mitandaoni.


Kupitia mitandao yake ya kijamii wa Instagram na Twitter  wa Nicky Bongozozo ameandika kuwa

"mama Jessica wangu nakupenda sana kwa zaidi ya miaka 20 na upendo wangu utakuwepo mpaka siku yangu ya mwisho, naomba msamaha kwa makosa yangu yote hasa kuropoka ropoka ovyo, Nilikosea ilibidi niweke maisha yetu "private" nisitangaze kwa watu millioni 30"
"Sijaridhika kabisa unavyoniambia watu wanakufuata "inbox" wanakutukana na kukuonea. suala la uonevu kwenye mtandao ni kubwa ila watu wajue wakionea familia yangu wamenionea mimi, mwendo wangu ni kujaribu kufurahisha watu si kuongelea Taifa Stars tu" ameandika Bongozozo
"Najitahidi kutoa burudani upande wa muziki, vituko, kucheza, na clips nyingine zinazoleta raha kama naona mama watoto wangu anaonewa, nitaacha kutoa hizo kumbukeni moyo si chuma, maneno mengine yanauma" ameongeza
Nicky Bongozozo amejipatia umaarufu kupitia mtandao wa Instagram, baada ya kuwa anaongea Kiswahili fasaha hali ya kuwa yeye sio mtanzania, huku akiishabikia timu ya Tanzania, kwenye mashindano ya Kombe la Afrika "AFCON" yaliyofanyika mwezi Juni hadi Julai mwaka 2019.