NEWS

9 Novemba 2019

Gigy jiwe lililokataliwa!

MSANII machachari kwenye Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema wakati anatoka kimuziki, watu wengi walimdharau na kumuona hafai, lakini ukweli ni kwamba, jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la pembeni. Gigy ambaye juzikati alikula shavu la ubalozi wa taulo za kike, ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, kwa sasa watu wanamuelewa na Mungu atazidi kumbariki.

“Watu walinichukulia poa na wengine walishindwa kunipa kazi wakiamini siwezi kuzifanya, lakini sasa Mungu ameniona, ninachoweza kusema ni kwamba jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la pembeni,” amesema Gigy.

Stori: Imelda Mtema, Dar

The post Gigy jiwe lililokataliwa! appeared first on Global Publishers.