NEWS

24 Novemba 2019

Jeshi La Polisi Lamsaka Mkufunzi Aliyesababisha mauaji ya Vijana wawili waliokuwa kwenye mafunzo ya Jeshi la Mgambo

Polisi Mkoani Singida wanamsaka Mkufunzi Msaidizi wa Jeshi la Akiba Said Ng'imba kwa tuhuma za mauaji ya Vijana wawili waliokuwa kwenye mafunzo ya Jeshi la Mgambo Kata ya Mudida Singida.

Kamanda wa Polisi Singida, Sweetbert Njewike amesema Wanafunzi hao wanadaiwa kufariki baada ya kupewa adhabu iliyopitiliza kwa kutakiwa watumbukie ndani ya dimbwi lililojaa maji ya mvua kitendo kilichopelekea wapoteze maisha kwa kushindwa kupumua.

Inadaiwa Mkufunzi aliwapa adhabu hiyo baada ya Wawili hao kutuhumiwa kutoshiriki ipasavyo mafunzo ya November 19 mwaka huu.

"Wanafunzi hao baada ya kutumbukia kwenye maji hawakuibuka, Mkufunzi akatoweka haraka na kukimbiia kusikojullikana, tunaendelea kumsaka"-Amesema