NEWS

26 Novemba 2019

Jux adai hawezi kumuongelea vibaya Vanessa Mdee


Msanii wa RnB nchini Tanzania, Juma Jux , amesema hawezi kumuongelea vibaya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Vanessa Mdee, hata kama wameachana na kila mtu kufanya maisha yake.


Jux amefunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, ambapo amesema licha ya kuachana kwao lakini bado yupo sawa na Vanessa Mdee pia hajamu 'unfollow' kupitia mitandao ya kijamii.

"Sioni sababu ya kumongelea vitu vibaya na kwanini nifanye hivyo na nisiongee vitu vizuri,  kwenye vitu vibaya na vizuri huwa nachagua vizuri siku zote, hayo ni maamuzi ya mtu au malezi ya mtu kwa sababu nimeshakuwa katika matukio mazuri na yeye kipindi cha nyuma na zilikuwa bora zaidi kuliko kipindi hiki" amesema Jux.

Jux na Vanessa Mdee wameachana miezi kadhaa iliyopita, ambapo sasa hivi kila mtu yupo katika mahusiano mapya.