NEWS

26 Novemba 2019

Wajue wanamuziki 10 wakubwa Afrika, Diamond yumo


Msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ametajwa kwenye orodha ya wasanii 10 wakubwa zaidi Barani Afrika Kwenye Orodha iliyotajwa na Shirika la Habari CNN pia wametajwa 'African Giants' wengine kama Burna Boy, Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Mr Eazi, Sho Madjozi, Busiswa Gqulu na Slapdee.

Diamond Platnumz ametajwa kwenye orodha hiyo kufuatia Ukubwa wa nyimbo zake na alizoshirikishwa pamoja na Matamasha aliyoyafanya na Tuzo mbalimbali alizowahi kushinda huku wakitolea mfano Tuzo za MTV EMA za Mwaka 2015 ambapo Diamond aliweka rekodi kwa kuwa masanii wa kwanza Afrika kushinda tuzo hizo mbili ndani ya Usiku Mmoja.

1. Burna Boy: Nigeria
2. Angelique Kidjo: Benin
3. Diamond Platnumz: Tanzania
4. Yemi Alade: Nigeria
5. Tiwa Savage: Nigeria
6. Wizkid: Nigeria
7. Mr.Eazi: Nigeria
8. Sho Madjozi:Afrika Kusini
9. Busiswa Gqulu: A. Kusini
10. Slapdee: Zambia