Kasi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa UKIMWI katika Jiji la Tanga yameshuka kutoka asilimia 5 ya 2017 hadi asilimia 2.2 Julai 2019
Mratibu wa UKIMWI Jijini Tanga, Mosses Kisibo amesema kupungua huko kunatokana na hamasa ya Elimu ya Upimaji wa Hiari waliyoitoa kwa jamii kuanzia ngazi ya shule za msingi
Kutokana na Elimu hiyo, sasa kasi ya watu kujitokeza kupima imeongezeka kutoka watu 51,344 mwaka 2017 hadi kufikia watu 66,308 mwaka 2018
Akiongelea uanzishaji wa dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo, alisema kuwa wamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 91 kuwaingiza waathirika katika matumizi ya dawa za ARVS