BOLIVIA
Meya wa Mji mmoja mdogo amevamiwa na Waandamanaji wa Upinzani ambapo alitembezwa mitaani bila viatu huku akiwa amepakwa rangi nyekundu na kisha kukatwa nywele kwa lazima
Meya huyo, Patricia Arce kutoka Chama Tawala alikabidhiwa kwa Polisi katika maeneo ya Vinto baada ya kukaa saa kadhaa na Waandamanaji hao
Tukio limetokea katika vurugu zinazoendelea baina ya Wafuasi wa Serikali na Wapinzani kufuatia kufanyika kwa Uchaguzi wa Rais wenye utata, na hadi sasa watu watatu wanadaiwa kufa
Wapinzani walifunga daraja huko Vinto, katika Mji Mdogo ndani ya Mkoa wa Cochabamba, ikiwa ni sehemu ya kuonesha kupinga uchaguzi uliofanyika Oktoba 20, 2019
Tetesi zilisambaa kuwa Waandamaji Wapinzania wawili waliuawa kati katika mapambano yaliyotokea karibu na Rais Mteule, Evo Morales , jambo lililozua hasira kwa Wapinzani
Wapinzania walimshutumu Meya Arce kwa kujaribu kuvunja vizingiti vyao walivyokuwa wameviweka dhidi ya wanaomuunga mkono Rais na pia walimshutumu kuhusika na vifo vya wenzao