NEWS

29 Novemba 2019

Polepole "Nimesikia Sumaye Hata Uenyekiti wa Kitongoji Wamembwaga, Akalee Wajukuu"



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amrushia kijembe Frederick Sumaya kwa kumuambia hata uenyekiti wa kitongoji amekosa Pwani.

Polepole alisema mzee Sumaye alipokuwa CCM walimpa upendeleo uwaziri mkuu miaka 10.

“Mzee nadhani muda umefika huko hakuna watu, mimi na wewe tunajua imetosha. Mwenzio amepumzika na muda wa kulea wajukuu anao,” aliandika ujumbe huo katika akaunti yake ya Twitter.

Aliandika ujumbe huo:” 
Nimesikia mzee Sumaye hata uenyekiti sijui wa kitongoji wamembwaga huko Pwani alipokuwa CCM tulimpa kwa upendeleo Uwaziri Mkuu miaka 10. Mzee nadhani muda umefika huko hakuna watu, Mimi na wewe tunajua imetosha. Mwenzio amepumzika na muda wa kulea wajukuu anao,” aliandika Polepole.


Uchaguzi uliofanyija jioni Kibaha Pwani wa kumpata mwenyekiti wa Kanda ya pwani, Chadema ulimalizika jana na matokeo kutangazwa.

Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mgombea alikuwa Mzee Sumaye peke yake ndipo zikapigwa kura za ndio au hapana

Matokeo ya kura za ndio kwa Mzee Sumaye ni 28, na kura za Hapana ni 48

Hivyo, nafasi ya Mwenyekiti bado iko wazi.