NEWS

29 Novemba 2019

Sumaye Apigwa chini Chadema..Adai Hajui Kama ni Adhabu



Aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani Friedrick Sumaye amepigwa chini katika nafasi hiyo hivyo ataendelea kuwa mwanachama wa kawaida.
Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchauzi huo ambapo alikuwa anapigiwa kura ndiyo na hapana amesema kama ni adhabu ameipokea.

Ili kushinda nafasi hiyo Sumaye alitakiwa kupata asilimia 50 ya kura zote lakini kati ya kura 73 zilizopigwa Sumaye amepata kura 28 tu za ndiyo na zilizosalia zilikuwa kura za hapana.

Akiwashukuru wajumbe amesema hata lililofanyika ni demokrasia japo hana uhakika kama ni adhabu amepewa kwani alichokifanya alitumia haki yake ya kikatiba,  kauli ambayo inaweza kuhusishwa na uamzi wake wa kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa Taifa wa Chama hicho.

“Nlikuwa natamani ningekuwa na mtu wa kumpongeza kazi yangu ya ofisi imeisha niwashukuru wale wote walionipa kura na wale amabao hawajanipa kura”amesema Sumaye
Amesema alitegemaea matokeo hayo toka alipoona taarifa kwenye gazeti jambo ambalo amelitaja kuwa halina afya kwa chama hicho lakini amesisitiza kuwa mambo mengine yatajulikana mbeleni.

Baada yakutangazwa kwa matokeo hayo baadhi ya wajumbe na mwanachama waliokuwepo waliibua shangwe na kuimba nyimbo mbalimbali za Chama chao wakisema mapambano bado yanaendelea.