NEWS

11 Novemba 2019

Rais Magufuli Afanya Uteuzi Mwingine

Rais Dkt. Jon Magufuli amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Pia, Dkt. Alexander Lugatona Kyaruzi ameteuliwa kuwndelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Wakati huo huo, Joseph Odo Haule anaendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) huku Dkt. Felician Bakamaza Kilahama akiendelea kuwa Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).

 

Aidha, Rais Magufuli amemteua Prof. Shadrack S. Mwakalila kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kipindi cha miaka miwili.

magufuli

The post Rais Magufuli Afanya Uteuzi Mwingine appeared first on Global Publishers.