Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Daniel Budeba kuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania – GST).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Budeba umeanza tarehe 15 Novemba, 2019.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Budeba alikuwa Mhadhiri wa Idara ya Uhandisi wa Kemikali na Madini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).