NEWS

30 Desemba 2019

Iran yalaani mashambulizi ya Marekani Iraq na Syria


Iran imelaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani nchini Iraq na Syria dhidi ya wanamgambo wa Kataib Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq, Abbas Mousavi amesema wanalaani vikali uchokozi wa Marekani katika ardhi ya Iraq na vikosi vya Iraq na wanauona kama mfano wa wazi wa ugaidi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper alisema jana vikosi vyake vilifanya mashambulizi yaliyowalenga wanamgambo wa Iraq wanaoungwa mkono na Iran, wakiwalaumu kwa shambulizi la roketi lililomuua mkandarasi wa Kimarekeni.

Esper amesema Marekani imeyashambulia maeneo  matatu ya magharibi mwa Iraq na mawili mashariki mwa Syria, ikiwemo maghala ya silaha na kambi zinazodhibitiwa na wanamgambo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema mashambulizi hayo ni ujumbe kwamba Marekani haitovumilia vitendo vyovyote vya Iran ambavyo vinahatarisha maisha ya Wamarekani.