NEWS

28 Desemba 2019

Islamic State Nigeria ‘Limewakata Vichwa Mateka Wakristo’


Moja ya stori ya kuifahamu leo December 28, 2019 ni kundi la Islamic State limetoa video linayodai inaonyesha mauji ya Wakristo 11 nchini Nigeria.

IS linasema kuwa mauji hayo ni sehemu ya kampeni yao ya hivi karibuni ya “kulipiza kisasi cha mauaji ya kiongozi wake na msemaji nchini Syria.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuwahusu wahanga, ambao wote walikua ni wanaume, lakini inasema walikua “wamekamatwa katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita” katika jimbo la kaskazini-mashariki mwa Nigeria la Borno.

Video hiyo ya dakika 56-ilitolewa na ”shirika la habari ”la IS Amaq.

Video hiyo imetolewa tarehe 26 Disemba na wachambuzi wanasema ni wazi imetolewa kwa makusudi katika kuambatana na sherehe za Christmas.