Wakazi wawili wa Kijiji cha Mseki kata ya Bulungwa Joseph Maweda (24) na Fabian Petro (20) wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kilo nane.
Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Christina Laurent Chovenye Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Evodia Baimo alidai kuwa wawili hao walitenda kosa hilo Aprili 21 mwaka huu katika eneo la Mwabomba .
Amefafanua kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kinyume na Vifungu 17(1)(b) na 2 namba 5 vya sheria ya kuzuia na kupamba na dawa za kulevya ya mwaka vya mwaka 2017.
Watuhumiwa hao wote kwa pamoja wamekana shitaka linalowakabili namba 132 la mwaka huu na limeahirishwa hadi Mei 25 mwaka huu litakapoanza kusikiliwa baada ya upelelezi wake kukamilika
Washitakiwa wote kwapamoja wako nje baada ya kukidhi Masharti ya dhamana ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja.
Mwisho.