NEWS

29 Aprili 2020

Mbunge wa Jimbo la Sumve Richard Ndassa amefariki dunia leo mkoani Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Sumve mkoani Mwanza, Richard Ndassa amefariki dunia leo Aprili 29, 2020 jijini Dodoma.

Ndassa ambaye ni mbunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amekuwa bungeni tangu mwaka 1995 hadi umauti ulipomkuta.

Katika utumishi wake wa Bunge la Tanzania amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo kuwa mjumbe wa kamati mbalimbali kama vile Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Maadili, pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini