NEWS

27 Aprili 2020

VIDEO: Mazishi ya aliyekua mkuu wa wilaya wa Mtwara Evodi Mmanda Kuhudhuriwa na Watu Wasiozidi 10

Mazishi ya aliyekua mkuu wa wilaya wa Mtwara Evodi Mmanda yatahudhuriwa na watu 10, na serikali ndio itasimamia mazishi hayo.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema familia ya marehemu imeridhia mwili kutosafirishwa hivyo marehemu atazikwa mkoani Mtwara.

Amesema lengo ni  kusimamia taratibu za wizara ya afya kuzuia mikusanyiko katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya corona.
 

Byakanwa amesema hayo leo Jumatatu April 27, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari huku akisisitiza kutokupuuza kufuata maelekezo ya wizara ya afya ya kijikinga na ugonjwa wa corona.
 
==>>Msikilize hapo chini