NEWS

21 Julai 2020

Huwezi Amini Watoto wa Nyerere Wapigwa Chini Vibaya Kura za Maoni....


Watoto wa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro na Madaraka Nyerere wameshindwa kutamba katika Jimbo la Butiama Mara, baada ya kupata kura za maoni chache.

Katika Wajumbe 555 waliopiga kura, kukiwa na wagombea 59,Makongoro alipata kura tano na Madaraka Nyerere aliambulia kura mbili.

Mshindi wa Jimbo hilo alitangazwa kuwa ni Jumanne Sagini aliyepata kura 84, akifuatiwa na Frank Mahemba aliyepata kura 80, wa tatu akiwa Joseph Nyamboha kura 46.