NEWS

14 Septemba 2020

Harmonize 'Upendo Wangu Juu ya DIAMOND Platnumz Mungu Ndio Anajua Pekee'

Harmonize amemtoa machozi Meneja wake Jembe ni Jembe baada ya kusimulia alivyolipishwa Mil 500 na menejimenti yake ya zamani iliyopo chini ya Diamond Platnumz.

Harmonize amesimulia kwamba wakati anaambiwa alipe hizo pesa hakuwa nazo ila Jembe alimpa kiasi cha shilingi mil 100 na yeye akaongezea mil 200 kwa kuuza baadhi ya vitu vyake alivyokuwa ameviwekeza nchini Italia kwa mke wake.

Mbali na hilo Harmonzie ameongeza kuwa kuna watu wengi sana wana waza kuwa Jembe yupo kwake kwa ajili ya pesa, amekanusha na kusema hilo sio bali Jembe ndio mtu alimfanya asimame mpaka hapa alipo.

Pia ameongeza kuwa yeye anampenda sana Diamond akimaanisha uongozi wake wa zamani na kusema upendo alionao juu ya uongozi huo mungu pekee ndio anajua.