NEWS

6 Septemba 2020

NCCR Mageuzi Wataja Vipaumbele 10 Endapo Watashinda Kiti cha Urais wa Tanzania



Chama cha NCCR-Mageuzi jana  kimezindua rasmi kampeni zake za Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Zakhiem-Mbagala jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa NCCR-Mageuzi akiwemo Mwenyekiti wake, James Mbatia.

Katika uzinduzi huo, Chama cha NCCR-Mageuzi kimewanadi wagombea wake katika Kiti cha Urais wa Tanzania na Makamu wa Rais. Yeremia Kulwa Maganja akiwa mgombea Urais huku Haji Ambar Khamis akiwa mgombea wake mwenza.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Maganja ametaja vipaumbele vyake 10 atakavyovifanyia kazi endapo atachaguliwa na Watanzania ikiwemo upatikanaji wa katiba mpya, elimu, mwafaka wa kitaifa, afya na ustawi wa jamii, mazingira na makazi, uhuru wa vyombo vya habari na asasi za kiraia.

Vipaumbele vingine ni usawa wa kijinsia, uchumi, ulinzi na usalama na vita dhidi ya rushwa