NEWS

14 Septemba 2020

Profesa Ibrahim Lipumba : Tutawekeza Katika Sekta Ya Afya na Elimu Endao Tutashinda Uchaguzi Huu

Chama cha Wananchi CUF kimesema endapo kitapata ridhaa ya kuongoza Serikali kutoka kwa wananchi kwenye uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu, Chama hicho kitawekeza kwenye rasilimali watu ikiwemo afya na elimu.

Hayo yamesemwa na mgombea urais kupitia chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Kilolo  mkoani Iringa jana kwenye mkutano wake wa kampeni.
 
Amesema kama watu hawana elimu na afya bora, ukiwekeza kwenye vitu vingine haitawasaidia chochote.

“Endapo tutapewa ridhaa Sera ya CUF itawekeza kwenye vitu muhimu vya afya na elimu ili viweze kuwasaidia Watanzania katika kujikwamua na umaskini,”amesema.

Kuhusu Muungano, Profesa Lipumba amesema muungano ni muhimu na endapo watachaguliwa wataimarisha Muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na pande zote kuwa na haki sawa.

Alisema watakapopata ridhaa hiyo ya kuongoza nchi wataendeleza muungano kwa kuwa ni muhimu kwa Taifa letu.