NEWS

9 Septemba 2020

Wanaodhani Nitajiondoa Katika Kinyang'anyiro cha URAIS wanaota ndoto za Mchana- Membe



Mgombea wa Urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo Bernard Membe, ameweka wazi kuwa hatojiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Membe ameweka wazi msimamo wake huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema kuwa wanaofikiri kuwa atajiondoa katika kinyang’anyiro hicho wanaota ndoto za mchana.

“Hatoki mtu hapa! Wale wote wanaodhani kuwa nitajiondoa katika kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, wanaota ndoto za Mchana.” Ameandika Membe.

Aidha Membe amewataka watanzania kukaa chonjo na kujiandaa na yatakayojiri kuanzia tarehe 15 Septemba 2020.

Ikumbukwe Jumatatu ya wiki hii mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu katika ufunguzi wa kampeni kanda ya Unguja, alisema vyama vya upinzani bara vinabidi viuunge mkono mtu anayeweza kuwa mshindani mzuri dhidi ya mgombea wa chama tawala visiwani Zanzibar.