Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi 3 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob
Viongozi hao wamekamatwa kwa madai ya kuhatarisha usalama wa Raia na mali zao kutokana na kupanga kuwatumia vijana kuchoma moto Miundombinu na Vituo vya Mafuta
Aidha, Mambosasa amewataka Wagombea Ubunge kutoka Mikoani walioshindwa katika Uchaguzi kurudi Majimboni mwao kwa sababu kitendo cha kukusanyika jijini humo ni uchokozi wa dhahiri kwa wakazi wa Dar
Jamii Forums