Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema itasimamisha mpango wake wa kuwapa chanjo dhidi ya COVID-19 wafungwa wa makosa ya ugaidi wanaozuiwa kwenye kambi ya Guantanamo kufuatia kuongezeka kwa malalamiko katika wakati ambapo nchi hiyo inajikakamua kuwachanja kwanza watumishi wa afya na wazee.
Msemaji wa wizara hiyo John Kirby ameandika hayo kupitia ukurasa wa twitter akisema hakuna mfungwa yoyote kwenye kambi hiyo ambaye tayari amechanjwa.
Kirby amekiri akisema ni kweli rais Joe Biden amesema ana mpango wa kutokomeza virusi vya corona katika siku yake ya kwanza ofisini lakini hakusema atawapa chanjo magaidi kwanza kabla ya Wamarekani.
Kambi ya Guantanamo iliyoko Cuba inawazuia washukiwa wa makosa ya ugaidi ikiwa ni pamoja na Khalid Sheikh Mohammed, mfuasi wa kundi la Al-Qaeda anayedaiwa kupanga shambulizi la Septemba 11.
-DW