Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Dar es Salaam
Tamasha la pili la Muziki nchini la Serengeti (Serengeti Music Festival) linatarajiwa kufanyika Februari 06, 2021 Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma litashirikisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa sasa na wa zamani (Bongo Fleva) ili kuwaburudisha watanzania ndani na nje ya Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema hayo leo jijini Dar es salaam kupitia mahojiano aliyofanya kupitia kipindi cha “Kakakuona” kinachorushwa na redio Clouds.
“Wizara tuna jukumu la kulea vipaji, wapo wasanii walioanzisha Bongo Fleva wakatengeneza njia ya hawa wasanii wengine kupata mafanikio, kama wizara tunaheshimu na tumeanzisha Serengeti Music Festival tamasha ambalo litazingatia kuwapa nafasi hawa pamoja na wasanii wapya kutoa burudani, karibuni tuburudike, Wizara hii kazi yake ni pamoja na burudani” alisema Waziri Bashungwa.
Aidha, Februari 05, 2021 Wizara imeandaa mkesha kabla ya kuelekea tamasha la Serengeti ambao utafanyika katika eneo la Royal Village jijini Dodoma ambapo Waziri Bashungwa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Waheshimiwa Wabunge pamoja na voingozi wengine ambao hawatapata fursa ya kuhudhuria tamasha lenyewe Uwanja wa Jamhuri.
Kupitia kipindi hicho, Waziri Bashungwa pia alizungumzia masuala mbalimbali yanayosimamiwa na wizara yake ikiwemo Habari ambapo amesisistiza wanahabari kuzingatia weledi na taaluma ya kazi yao huku akisisitiza wa Serikali inaendelea kuisimamia Sheria ya Hudma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 ambapo amesema kabla ya mwaka 2021 kuisha, wizara yake itahakikisha imeunda Bodi ya Ithibati na Baraza la wanahabari ili kutoa nafasi kwa wanahabari kujadili changamoto zinazowakabili pamoja na utatuzi wake.
Katika kipindi hicho, Waziri Bashungwa alizungumzia masuala mbalimbali yanayosimamiwa na wizara yake ikiwemo Habari ambapo amesisistiza wanahabari kuzingatia weledi na taaluma ya kazi yao huku akisisitiza wa Serikali inaendelea kuisimamia Sheria ya Hudma za Habari Na. 12 ya mwaka 2026 ambapo amesema kabla ya mwaka 2021 kuisha, wizara yake itahakikisha imeunda Bodi ya Ithibati na Baraza la wanahabari ili kutoa nafasi kwa wanahabari kujadili changamoto zinazowakabili pamoja na utatuzi wake.
“Jukumu la Wizara ni kusimamia nidhamu, inapotokea chombo chochote cha habari au msanii kufungiwa inakuwa wamefikia hatua ambayo hata mimi kama mzazi nimefikia mwisho ndio maana hata lilipotokea ukiukwaji wa maadili ya jamii na taaaluma kwa wanahabari ama chombo cha habari huwa tunakaa kujadili tunawasaidia vipi na ninaamini huwa tunawasaidia” alisema Waziri Bashungwa
Kuhusu ukuaji wa sekta ya Sanaa na Michezo nchini, Waziri Bashungwa amesema kuwa wizara anayoiongoza tayari wanamajadiliano na Wizara ya Fedha na Mipango kupata nafuu kwaajili ya vifaa vya michezo ili kusaidia sekta ya michezo na vifaa vyake vipatikane kwa urahisi na kwa bei nafuu hatua itakayosaidia kuboresha viwanja kwa kushirikiana na sekta binafsi ili hatimaye kuinua vipaji vya wanamichezo mbalimbali nchini na kuwaonmgezea mapato yao na taifa kwa ujumla.
Katika kuhakikisha michezo nchini inakuwa yaenye tija Serikali itajenga uwanja Changani jijini Dodoma “Sports Arena” itayohusisha michezo mbalimbali ili kuinua viopaji vya wanamichezo kuanzia ngazi ya shule za msingi na sekondari kwa vijana wadogo hatimaye kuwa na timu imara za taifa ambazo zitaleta heshima ndani na nje ya nchi.
“Tunazungumza na Shirikisho la Soka nchini TFF ili wafanye utafiti wa namna ya kuweza kuwaendeleza vijana wenye vipaji lakini wakiwa katika mfumo usio rasmi hususani baada ya kumaliza shule ya msingi, kidato cha nne ama cha sita ili kuhakikisha hatuna kipaji chochote tunachokipoteza,” alisema Bashungwa.
Kwa upande wa Sanaa, Waziri Bashungwa amesema kuwa ameshakaa na Bodi ya Filamu kuwaelekeza kuwajengea uwezo wasanii wa filamu hatua itakayowazalisha filamu zinatengenezwa nchini ziweze kuuzika ili kuikuza Bongo Movie na kuifanya filamu hizo zitaweza kushindana katika soko huria.