NEWS

29 Aprili 2021

Rais Samia Suluhu Hassan kupigiwa kura kuwa Mwenyekiti CCM


Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimependekeza jina la Rais Samia Suluhu Hassan kupigiwa kura kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma hii leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, – Humphrey Polepole amesema kuwa jina la Rais Samia Suluhu Hassan limeungwa mkono na Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM.

Amesema kuwa, jina hilo litapelekwa kwenye mkutano mkuu maalum.wa CCM utakaofanyika hapo kesho, ili Wajumbe wa mkutano huo walipigie kura.