Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka 27 bilionea mkubwa duniani kwa mujibu wa jarida ya Forbes, Bill Gates na mkewe, Melinda wametangaza kupeana talaka.
“Hatuamini tena tunaweza kuwa pamoja kama wanandoa. Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu," wameeleza.
"Katika kipindi cha miaka 27 iliyopita tumewalea watoto watatu wa ajabu na kujenga wakfu ambao unafanya kazi ulimwenguni kote kuwezesha watu wote kuishi maisha yenye afya, yenye tija.”
"Tunaendelea kuwa na imani ya pamoja katika lengo hilo na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwenye wakfu wetu lakini hatuamini tena tunaweza kukua pamoja kama wanandoa katika sehemu inayofuata ya maisha yetu.
Tunaomba nafasi na faragha kwa familia yetu tunapoanza maisha haya mapya,” wameeleza kupitia mtandao huo.
Melinda aliyejiunga na kampuni ya Bill ya Microsoft mwaka 1980 na Gates wana watoto watatu.