NEWS

22 Juni 2021

Mahakama yatengua uamuzi wa Fatma Karume kufutiwa uwakili


Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Mawakili, ambayo ilimfuta Uwakili, Fatma Karume na kuagiza uamauzi huo uliotokana na malalamiko yaliyotolewa na Mwanasheria Mkuu yapelekwe kwenye kamati hiyo na Fatma apate nafasi ya kujitetea.

Fatma Karume alisimamishwa Uwakili Septemba 20, 2019 na Mahakama Kuu kwa madai ya kuishambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika uamuzi huo uliotolewa na Jopo la Majaji watatu imebainisha kuwa Mwanasheria Mkuu hakuwa na mamlaka ya kupeleka malalamiko kwenye Kamati ya Maadili isipokuwa Msajili wa Mahakama.

Kutokana na hatua hiyo, uamuzi umebainisha kwamba unamrudishia Fatmah katika orodha ya Uwakili ila ataendelea kusimamishwa uwakili kama amri ya Jaji Dr. Elieza Feleshi hadi hapo atapojitetea mbele ya Kamati hiyo.