NEWS

21 Juni 2021

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon 'Nikki wa Pili' Afunguka Baada Ya Kuapishwa

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon 'Nikki wa Pili' amefunguka baada ya kuapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kuwa Mkuu wa wilaya hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nikki wa Pili ameandika kuwa  "Kwanza namshukuru Mungu, pili Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, MHe. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Kisarawe na Serikali

"Nina ahidi kutumia vipawa vyangu, busara zangu na uwezo wangu kuifanya kazi hii nikishirikiana na watumishi wenzangu pamoja na wananchi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Shukrani kwa wote walio nitumia salamu za pongezi na mimi nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano"