Hapa nitakuelekeza mambo yote unayotakiwa kuyafanya unapoandika barua ya maombi ya kazi. Jifunze taratibu ili baadaye uweze kuandika barua unayotaka na uweze kupata kazi
_____ii. Tarehe.
iii. Anuani ya anayeandikiwa.
iv. Salamu.
v. Kichwa cha habari.
- Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.
- Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani, hayana msaada.
- Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?
vii. Mwisho wa barua. Mwisho wa barua yako uwe na:
- Sahihi yako.
- Jina lako
__________
Mfano huu wa barua ni wa barua ya maombi ya kazi ya ualimu. Hata hivyo, muundo huu unaweza kutumika katika kuomba kazi yoyote.
Mtaa wa Mawe
S.L.P 000,Manyara.
0700000000.
10/07/2021.
Mkuu wa shule,
Shule ya sekondari Mawe,
S.L.P 0000,
Manyara.
Ndugu,
YAH: OMBI LA KAZI YA UALIMU WA KISWAHILI NA HISTORIA
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24. Ninaomba kazi ya ualimu katika shule yako kama ilivyotangazwa katika gazeti la Mpekuzi siku ya Jumamosi tarehe, 10-07-2021.
Nimehitimu shahada yangu ya ualimu kwa masomo ya Historia na Kiswahili mwaka 2019 katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Pia nimefanya kazi ya kufundisha kwa miezi mitano katika shule ya wasichana Kitambi iliyoko Mbuyuni. Mbali na hayo, nina uwezo mkubwa wa kutumia kompyuta.
Uzoefu wangu wa kazi na elimu niliyonayo, vinanishawishi niamini kuwa, ninafaa kufanya kazi katika shule yako. Pia, ninaahidi kufanya kazi kwa bidii ili niweze kufikia malengo ya shule ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaofeli mitihani yao.
Ninategemea majibu mazuri kutoka kwako na nipo tayari kwa usahili siku yoyote nitakayohitajika. Kwa uthibitisho zaidi, nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu.
Wako mtiifu,
Sahihi
Maneno Kitunguu
___________
Huo ni mfano wa Barua ya maombi ya kazi kwa Lugha ya Kiswahili.
==>>Kupata Mifano zaidi ya 50 ya Barua ya Maombi ya Kazi kwa Lugha ya Kiingereza, Bofya hapo chini kulingana na taaluma yako uliyosomea.
_______
1. Cover Letter Sample for Qualified Teacher
2.Cover Letter Sample for a French Teacher
3.Cover Letter Sample for Economist
4.Cover Letter Sample for an Insurance Graduate
5.Cover Letter Sample for Administrative Officer
6.Cover Letter Sample for Human Resource Manager
7.Cover Letter Sample for Marketing Executives
8.Cover Letter Sample for a Law Graduate
9.Cover Letter Sample for Psychologist
10.Cover Letter Sample for Accounting Graduate
11.Cover Letter/Resume Sample for Computer Science