Akiongea na Millardayo.com Diamond alisema pamoja na kufanya wimbo na Davido, alimshirikisha pia Iyanya kwenye wimbo mwingine kabisa japokuwa watu wengi hawafahamu kuhusu collabo hiyo.
Alisema lengo lake kubwa lilikuwa si kufanya collabo tu bali anasema alitaka kujenga ukaribu na wasanii wa Nigeria na ndio ameamua kwenda kufanya video huko huko.
