“I asked my doctor if anybody has ever been admitted in hospital for smoking weed .He said ,NO! So f**k what everybody thinks. Do what makes u happy!” Aliandika Huddah kwenye kwenye post ya picha ya kwanza akiwa anavuta marijuana.
Baada ya muda alipost picha nyingine akiwa na mavazi tofauti ikionesha kuwa ni siku ama mahala pengine, akiwa anamalizia kipisi cha bangi, na kuisindikiza na mashairi ya wimbo wa Wizkid ‘The Matter’.
“Dem swear dem bad ,but I swear dem do NUTTIN’ o weh! (LMFAO!)…… Oya ,back to did matter open and close ,touch your toes.Baby Oya yo di! #wizkid.”
Followers wake wengi walikilaani kitendo hicho na wengine kuonesha huruma kwa kile anachofanya.
“Who do u inspire with ua shoddy behaviours…#Not hating but please do meaningful stuff.” Aliandika follower mmoja anaetumia jina la vqeebent kwenye Instagram.
Mwaka jana Huddah alikiri kuwa aliwahi kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya hapo awali ikiwa ni pamoja na cocaine, na kwamba ilimvuruga lakini aliweza kwenda rehab na kupata matibabu sahihi. Sasa ameanza kuirudia hali hiyo taratibu kwa kunza na dawa za kulevya aina ya bangi.
Mungu amsaidie asiifikie hali ya kubwia unga iliyomtesa enzi zile na ambayo inaendelea kuwatesa wengi.