NEWS

11 Januari 2014

Mimo: App ya simu inayofuatilia upumuaji, ulalaji na joto la mtoto mchanga

Wazazi wapya sasa wanaweza kuwa na suluhisho la woga wao unaotokana na ulalaji wa watoto wachanga kwenye chumba chao wenyewe kwa mara ya kwanza.

Kusaidia kupunguza sehemu ya pressure hizi, kundi la wazazi kutoka Boston limeanzisha app ya simu iitwayo Mimo inayoweza kufuatilia upumuaji wa mtoto, joto na namna anavyojigeuza.

Taarifa zote hizi hutumwa kwenye app ya smartphone na zinaweza kutumiwa kwa aidha kuwahakikisha wazazi kuwa kila kitu kiko sawa ama kuwashtua iwapo kuna tatizo.

  
   
Mfumo wa Mimo unapatikana kwaajili ya watoto wanaoanzia siku moja hadi miezi 12 itaingia sokoni mwezi ujao.

By DAILY MAIL