Mhandisi Paul Mhangilwa Masanja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Paul Mhangilwa Masanja kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Obeni Y. Sefue mjini Dar Es salaam, Ijumaa, Januari 17, 2014, imesema kuwa uteuzi huo wa Bwana Masanja ulianza Januari 16, 2014.
Taarifa hiyo imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Masanja alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).