Hata hivyo mawaziri hao waliojiuzulu wanasalia kuwa wasimamizi wa wizara zao hadi pale serikali mpya itakapo buniwa.
![]() |
| RAISI WA UKRAINE |
Kura ya kuifutilia mbali sheria hio ilipigwa na asilimia kubwa ya wabunge wa taifa hilo. Sheria hio ilipiga marufuku waandamanaji kutumia majengo ya umma pamoja na kuvaa vinyago.
Mwandishi wa BBC nchini Ukraine, amesema kuwa upinzani utaiona hatua ya waziri mkuu kujiuzulu pamoja na kufutilia mbali sheria inayozuia maandamano kama ushindi kwao'
![]() |
| WAZIRI MKUU WA UKRAINE ALIYESTAAFU |
Waandamanaji hata hivyo wameapa kuendelea kuandamana hadi Rais Yanukovych atakapojiuzulu.

