NEWS

26 Machi 2014

Ile Video ya wasanii 22 wa Afrika kuhusu mradi wa ‘Do Agric’ ‘Cocoa na Chocolate’ kutoka March 31

Ile Video ya wimbo uliofanywa na wasanii 22 wa Afrika kuhusiana na kampeni ya ‘Do Agric’ ya mradi wa One Campaign uitwao, ‘Cocoa na Chocolate’ itatoka March 31.




Video na wimbo huo vilifanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini ambapo D’Banj aliongoza wasanii wengine wakiwemo Buffalo Souljah (Zimbabwe), Judith Sephuma (South Africa), Vusi Nova (South Africa), Liz Ogumbo (Kenya), Nancy G (Swaziland), Dama Do Bing (Mozambique), Diamond (Tanzania), Femi Kuti (Nigeria), Rachid Taha (Algeria), Juliani (Kenya), Omawumi (Nigeria), Tiken Jah Fakoly (Cote d’Ivoire), Fally Ipupa (DRC), Kunle Ayo (Nigeria), Wax Dey (Cameroon), Victoria Kimani (Kenya), Ambwene Allen Yessayah (Tanzania), na Dontom (Nigeria).

Wimbo ulitayarishwa kwa ushirikiano wa Cobhams Asuquo na DeeVee wa DB Records huku video ikifanywa na Godfather Productions.