NEWS

26 Machi 2014

Picha: Bongo Movie Unit watoa misaada kwa hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar Esa salaam

Wasanii wa Bongo Movie Unit leo wametembelea katika wodi ya akinamama na watoto katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa vitu wenye thamani ya shilingi milioni 15 kama njia ya kuishukuru jamii kwa mafanikio yao.

JB wakiwa na akinamama yenye watoto wodini

Steve na JB akiwa wakiwa na akinamama yenye watoto wodini



Mwenyekiti wa Bongo Movie Unit,Steve Nyerere amesema wameamua kufanya hivyo ili kurudisha walichokivuna kwa jamii.

“Tunaamini tunapata kipato kikubwa kutokana na filamu zetu na wateja wetu wa kuu ni akinamama,” Steve ameiambia Bongo5. “Kwahiyo tukaona tunatakiwa wakati tunatimiza miaka mitatu tangu bongo movie ianzishwe, tuwatembelee akinamama katika ma hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam na kutoa misaada, ndio tukaanza na hospitali ya MwananyaMAla,tukatoa misaada ya vitu mbalimbi kama nguo za watoto,mabeseni, yaani tumeangalia mahitaji yao kwa ujumla. Kwahiyo leo tumetoa msaada wa vitu vyenye thamani ya kama milioni 15.”