NEWS

18 Aprili 2014

Johari amkana Ostaz Juma na Ray, asema hana mpenzi

Staa wa filamu hapa Bongo, Blandina Changula ama Johari kwa jina maarufu, kufuatia ripoti mbalimbali kuhusiana na swala zima la mahusiano yake ya kimapenzi kushika chati katika siku za karibuni, ameamua kutoa kauli rasmi kuhusiana na swala hili.

Johari
Johari katika maelezo yake, amekana kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ray ambaye ni msanii na patna wake wa kibiashara, vilevile amekana kuwa katika ugomvi na msanii mwenzake Chuchu Hans, na vilevile akakana kuhusiana na swala la yeye kutaka kuolewa na Ostaz Juma.
Johari amesema kuwa, anawataka mashabiki wake kutokuamini maneno wanayoyasikia mtaani kila siku huku akiweka wazi kuwa, katika swala la mahusiano yeye kama mwanamke mwenye maadili ya ki-Afrika, hawezi kutangaza swala la mahusiano kwake kabla halijawa rasmi katika hatua ya uchumba.