NEWS

18 Aprili 2014

Wizkid amsimamisha kazi Meneja

Staa wa muziki kutoka nchini Nijeria, Wizkid ameripotiwa kusimamisha mkataba wa kazi na aliyekuwa meneja wake, Godwin Tom kufuatia kupishana maelewano na kuingia katika ugomvi mwishoni mwa wiki.



Kufuatia ugomvi huu, tayari msanii huyu katika mitandao amekwishabadilisha taarifa kuhusiana na msimamizi wa kazi zake na kuondoa jina la Tom, na vilevile Tom naye kwa upande wake amefuta rekodi zilizokuwa zinaonyesha anafanya kazi za Wizkid.

Sababu hasa ya ugomvi wa Staa huyu na meneja wake huyo wa muda, bado hazijawekwa wazi, isipokuwa kinachoonekana sasa ni kwamba wawili hawa wameamua kuacha kufanya kazi pamoja huku kila mtu akichukua njia yake, kukiwa hakuna matumaini yoyote ya kusuluhisha tatizo na kurejea kuendelea kufanya kazi pamoja.