NEWS

1 Mei 2014

Nikiwa 'single', sina bei-Halima Mdee

Mbunge wa jimbo la kawe jijini Dar es Salaama katika tiketi ya Chadema Mh. Halima Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa huwa hana bei pindi awapo Single,



Mdee amesema hayo kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachokukutanisha na mtu maarufu katika tasnia fulani kila siku za Jumatano.
Halima Mdee alikuwa akijibu moja ya swali aliloulizwa na shabiki wa ukurasa huo aliehitaji kujua gharama zake za mali kama anahitaji kumuoa na kuwa mke wake
"Mhe Kama nataka nikutolee Mali niandae Tsh ngapi? Halima Mdee:Nashukuru..ila siko single. Kama ningekuwa single ,huwa sina bei kabisaa"
mbali na hilo Mdee ameweka wazi mpango wake katika jimbo la Kawe kwa mwaka 2015 kuwa anaweza kugombea katika jimbo hilo ikiwa mwenyezi mungu atamjalia uzima na kama ataona utumishi wake bado unahitajika katika jimbo hilo na wananchi, na kusema kuwa chama chake cha Chadema kipo imara licha ya changamoto mbalimbali walizopitia.
"Kawe nitagombea kama mwenyezi mungu ataniweka hai...na kama nikiona kwamba utumishi wangu bado unahitajika na wananchi.Ila Chama kiko imara,japo tumepita katika kipindi kigumu kwa kila mmoja wetu.Naamini tutaimarika zaidi..changamoto na misukosuko unaifanya taasisi au mtu kuwa imara zaidi.
MCHAKATO WA KATIBA;

Maswali mengi yaliyoulizwa na mashabiki yalikuwa yakilenga katika kujua na kufahamu mustakabali wa mchakato wa Katiba na kujua kama Waakilishi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaweza kulejea bungeni kama ambavyo wamekuwa wakiombwa na baadhi ya viongozi wa Nchi kurudi kuendeleza mchakato huo,Mdee alisema kuwa kama wajumbe walio wengi wataacha kujadili rasimu ya Chama Cha Mapinduzi.
"Tutarudi kama walio wengi wataacha kujadili rasimu ya CCM....kilichotupeleka pale ni rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume....na si vinginevyo."
Shabiki mwingine alihitaji kujua kama Halima Mdee atakuwa teyari kukubaliana na suala la kubadili sheria ya mabadiliko ya katiba na jibu lake lilikuwa kama hivi
"Hatuwezi kuruhusu...itakuwa kuhalalisha matakwa ya kundi fulani kwa maslahi ya kundi husika. Sheria haina tatizo lolote...tunachotakiwa kama wajumbe wa bunge la katiba ni kutekeleza wajibu wetu kama sheria inavyotaka."