NEWS

23 Juni 2014

Ben Pol kuachia wimbo mpya July 27, umeandikwa na mwalimu wa chuo kikuu

Mwimbaji wa RnB Tanzania, Ben Pol ametangaza kuachia wimbo mpya alioupa jina la Upendo, July 27 mwaka.

Wimbo huo umeandikwa na mwalimu wa St. Augustine University of Tanzania (SAUT), anaefahamika kwa jina la Wynjones Kinye ambaye anafundisha masomo ya Mawasiliano ya Umma.


Mbali na kuwa mwalimu, Kinye pia ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo.




‘Upendo’

Siku hiyo (July 27) Ben Pol anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake ‘Unanichora’ aliomshirikisha Joh Makini. Imeiongozwa na Nisher ambaye tayari ameanza kutoa kionjo kupitia mitandao ya kijamii.